Alhamisi , 6th Oct , 2022

Jeshi la Polisi mkoani Mtwara linamshikilia Somoe Mohamed mwenye umri wa miaka 34,   mkazi wa kata ya  Dihimba, halmashauri ya wilaya ya Mtwara, kwa tuhuma za kumchoma  moto mwanae  mwenye umri wa miaka mitano kwa kosa la kuiba dagaa

Akizungumza na waandishi wa habari kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Humo, Nicodemus Katembo amesema Tukio hilo lilitokea tarehe 30/09/2022 majira ya saa 16:00 katika kijiji cha Namanjele ambapo Mtuhumiwa alitenda kosa hilo kwa kuweka nyasi kavu katikati ya viganja vya mikono ya Mtoto huyo kisha akamfunga kamba mikononi na kuwasha moto kwa kutumia kiberiti

Inaelezwa kuwa Mtoto huyo alifanyiwa ukatili huo baada ya kutuhumiwa kuiba dagaa na kwa sasa yupo chini ya uangalizi wa Afisa Ustawi wa Jamii wa Mtwara Vijijini na anaendelea kupatiwa matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Ligula

Aidha katika tukio la pili kaimu kamanda Nicodemus Katembo amesema Jeshi hilo linamshikilia Thomas simba mkazi wa Milyembe kata ya Moma kwa tuhuma za kumlawiti  mtoto wa miaka miwili