Jumapili , 25th Jul , 2021

Katika kumuenzi aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano Hayati Dkt. John Pombe Magufuli, wilaya ya Chato inakuja na maonesho ya utalii na wafanyabiashara yatakayofanyika wilayani humo kwa muda wa siku tisa.

Aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano Hayati Dkt. John Pombe Magufuli

Mkuu wa Wilaya hiyo Martha Mkupasi amesema lengo ni kuonesha utalii wa hifadhi za Burigi Chato, Kisiwa cha Rubondo na kukuza biashara na kutokana na mkoa wa Geita kupakana na nchi mbalimbali hivyo kupitia maonesho hayo kutakutanisha zaidi ya wafanyabiashara 400.

Zaidi Tazama Video hapo chini