Jumatatu , 6th Mar , 2023

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan anatarajia kuwa mgeni rasmi katika mshindano ya 23 ya kimataifa ya kuhifadhi quran tarehe 9,04,2023 kwenye uwanja wa Uhuru.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan

Mashindano hayo yanawashirikisha vijana kutoka bara la ulaya,America,Asia na Africa huku Tanzania ikiwa ndio mwandaaji kupitia taasisi ya Alhikma.

Awali akitoa nasaha kuelekea mashindano hayo sheikh mkuu na mufti mkuu wa Tanzania Abubakar Bin Zuberi amesema mashindano hayo yatakwenda sambamba dua za kuliombea Taifa kulinusuru na gadhabu ya Allah kutokana na matendo yanayotendwe kinyume cha maagizo yake.

Aidha mufti amewata waislam kote nchini kuitumia elimu ya dini na uwezo walionao kuhifadhi quran kutenda mema na kuleta athari chanya katika jamii.

Aidha mratibu wa mashindano hayo Sheikh Nurdin Kishik Amesema tayari Wamepata uthibitisho wa uwepo wa Rais na kuwataka watanzania kujitokeza katika uwanja wa uhuru ili kuchagiza mashindano hayo sambamba na kupata elimu ya Allah.