Jumaa Aweso-Waziri wa Maji
Akiwasilisha hoja za mkutano huo utakaoanza march 8,2023 Mkuu wa chuo cha maji Dkt Adamu Karia amesema Dunia iko na changamoto kubwa ya maji kutokana na mabadiliko ya tabia nchi hivyo kupitia kongamano hilo na mawasilisho kutoka kwa wataalamu wa maji duniani wanatarajia kubadilisha mfumo mzima wa maji ya asili na kuitazama kwa jinsi gani teknolojia na watalaam wamezalisha maji kwa kiasi gani kwenye mazingira.
Amesema Maji ni maisha ya kila mmoja na kwamba Mabara yote yamealikwa dunia wakionesha teknolojia zao ambapo jumla ya nchi 29 zitawasili ambapo mawasilisho zaidi ya 70 yatawasilishwa mgeni rasmi akitarajiwa kuwa waziri wa maji Jumaa Aweso.
Mwezi wa nne mwaka wa jana 2022 wizara iliandaa kongamano kubwa ambalo limezaa matunda makubwa ya mifumo,wataalamu na tafiti zenye manufaa kwa watanzania ikiwemo gunduzi mbalimbali za maji katika mifumo.







