Ijumaa , 8th Jul , 2016

Walimu wa shule za msingi zilizopo katika Halmashauri ya Manispaa ya Tabora, wametakiwa kuwa wabunifu katika ufundishaji ili kuziwezesha shule zao kuwa na maendeleo ya kielimu.

Aliekua Mkurugenzi wa Manispaa hiyo ambae sasa anahamia Jiji la Dar es Salaam, Sipora Liana.

Aliekua Mkurugenzi wa Manispaa hiyo ambaye sasa anahamia Jiji la Dar es Salaam, Sipora Liana, amesema matokeo mabaya ya wanafunzi wanaomaliza elimu ya msingi wilayani humo yanatokana na walimu kutotekeleza wajibu wao ipasavyo.

Akizungumza na walimu wa Masomo ya Hisabati, Kingereza na Kiswahili wa Halmashauri hiyo waliopatiwa mafunzo ya kujengewa uwezo, Bi. Liana amesema ili kupata matokeo mazuri lazima walimu wabadilike kifikra na kuacha kufanya kazi kwa mazoea.

Kwa upande wake Afisa Elimu Mkoa wa Tabora Emanuel Malima, yanalenga kutoa elimu bora kwa wanafunzi ikiwa ni pamoja na kukabiliana na changamoto ya elimu ya mkoa huo.

Nae Meneja wa Mamlaka ya Elimu nchini TEA, Musa Nzenga, amesema lengo kuu la mpango huo ni kuobresha elimu katika ngazi ya msingi lakini pia kuboresha ufaulu katika masomo yaliyochaguliwa kufundishwa.