Alhamisi , 17th Dec , 2015

Aliyekuwa mgombea wa urais kwa tiketi ya Chama cha ACT-Wazalendo Mama Anna Mghwira amewataka mawaziri kumshauri Rais katika kazi zake na sio kuelekezwa kufanya shughuli zao

liyekuwa mgombea wa urais kwa tiketi ya Chama cha ACT-Wazalendo Mama Anna Mghwira,Picha na Maktaba

Aliyekuwa mgombea wa urais kwa tiketi ya Chama cha ACT-Wazalendo Mama Anna Mghwira amewataka mawaziri kumshauri Rais katika kazi zake na sio kuelekezwa kufanya shughuli zao, huku wengine wakifanya kazi kwa kuiga kasi ya rais bila ya kuwa na viwango na ufanisi katika kile wanachokifanya.

Akizungumza na East Africa Radio katika mahojiano maalum Mama Mghwira ambaye pia ni mwenyekiti wa chama hicho amesema Rais, Dkt. John Magufuli ameanza na kasi pamoja na viwango ambavyo mawaziri wake wanahitajika kwenda nayo sambamba ili kuleta maendeleo na kutatua kero za wananchi kwa haraka.

Aidha, Mama Anna amemshauri Rais Magufuli kuteua mawaziri makini katika wizara nne nyeti zilizobaki ambazo zinabeba uchumi wa nchi katika kugundua matatizo yanayoikabili nchi kwa sasa na kuyatafutia ufumbuzi kwa haraka.