Jumatano , 16th Nov , 2022

Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Dkt. Pindi Chana, ameshiriki kikao kazi cha kujadili mkakati wa kulinda vyanzo vya maji na maeneo yaliyohifadhiwa, kilichoongozwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Selemani Jafo kwa Niaba ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.

Mawaziri wakiongozwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Selemani Jafo

Awali akimkaribisha, Waziri Jafo kuzungumza na wananchi, Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Dkt. Pindi Chana amesema Mto Ruaha ni tegemeo kubwa katika sekta ya Maliasili na Utalii hivyo ni vyema wananchi wakatunza misitu, kuacha kuchoma moto misitu ili kulinda mto huo na vyanzo vingine vya maji nchini.

Mawaziri wengine waliohudhuri kikao hicho ni pamoja na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angelina Mabula, Mashimba Ndaki, Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Anthony  Mavunde, Naibu Waziri wa Kilimo, Festo Dugange, Naibu Waziri Ofisi ya Rais  TAMISEMI.

Pamoja na Mawaziri hao pia kilihudhuriwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Prof.Eliamani Sedoyeka, Wakuu wa Mikoa,  wakuu wa wilaya na wataalam mbalimbali.