
Aliyekuwa Mbunge wa Singida Kaskazini Lazaro Nyalandu.
Kauli hiyo ameitoa wakati akizungumza na www.eatv.tv juu ya kupata wakati mgumu katika utekelezaji wa majukumu yake kutokana kuwa ni miongoni mwa wabunge ambao walipigiwa kura na wananchi wachache.
Monko amesema "changamoto kubwa niliyokumbana nayo ni kubadilisha aina ya uongozi kati ya mtangulizi wangu na namimi, na yule alikuwa na nguvu kwa sababu alikuwa madarakani, lakini wananchi ni walewale ambao wananiunga mimi mkono,"
"Ila kwa sasa hivi hawezi kuwa na nguvu, kwa sababu sio Mbunge ndiyo maana sasa hivi wananchi wamehamia kwangu, sasa sijui huko CHADEMA ana wananchi wangapi," ameongeza.
Kuhusiana na uchaguzi wa 2020 Mbunge huyo amedai anamsubiri kwa hamu Lazaro Nyalandu ili apambane naye tena.
"Tena ninamsubiri kwa hamu hiyo 2020, alitakiwa aingie juzi tupambane na kwa kweli kwa sasa Singida Kaskazini hana nafasi tena labda akagombee jimbo lingine".
Mwaka 2017 Lazaro Nyalandu akiwa Mbunge wa Jimbo la Singida Kaskazini alitangaza kujiuzulu kwa madai kuminywa kwa demokrasia nchini.