
Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Dodoma, Mariam Ditopile
Hayo ameyasema jijini Dodoma katika mkutano wake na wandishi wa habari ambapo amesema kwa kipindi kifupi cha serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan, mageuzi makubwa yamefanyika katika sekta ya kilimo kulinganisha na miaka ya nyuma ambapo kilio kikubwa kilikuepo.
"Tunamshukuru Rais Samia na serikali yake kwa usikivu wao kwetu sisi wakulima kwa kutuletea mfumo mzuri wa mbolea ya ruzuku pamoja na kutoa kipaumbele kwa wazalishaji wa ndani ili kulinda viwanda vyetu, ajira na usalama wa chakula," amesema Mbunge Ditopile
Amesema Rais Samia ndani ya muda mfupi amewezesha kupatikana kwa bajeti bora ya kilimo ambapo kwa mwaka huu wa fedha 2022/23 Wizara ya Kilimo imetengewa shilingi bilioni 751 huku shilingi bilioni 631 zikielekezwa kwenye miradi ya maendeleo.
Mbunge Ditopile ameongeza kuwa ongezeko la bajeti ya kilimo kwa mwaka huu wa fedha ni takribani asilimia 300 kulinganisha na bajeti ya mwaka 2020/21 ambapo kiasi kilichotengwa ni shilingi bilioni 229 na kati ya fedha hizo ni shilingi bilioni 150 pekee ndio zilienda kwenye miradi ya maendeleo.