Halima Mdee
Uamuzi huo umetolewa hii leo Septemba 2, 2022 na Jaji Cyprian Mkeha, wakati akitoa uamuzi kuhusiana na mapingamizi yaliyowasilishwa na wapeleka maombi
Jaji Mkeha baada ya kutoa uamuzi huyo, mjibu maombi wa kwanza, Wakili Peter Kibatala, aliiomba mahakama hiyo iwape dakika 15 ili aweze kujadiliana na wenzake.
Kabla ya kuahirisha shauri hilo kwa muda, Jaji Mkeha alimtaka Kibatala ashauriane na mjibu maombi namba mbili ambaye ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Tume ya Taifa ya Uchaguzi, kama watakubaliana kuendelea na kesi hiyo kwa muda huu au watakubaliana kuiahirisha.