Alhamisi , 9th Jun , 2022

Mzee Joseph Gendamwene (80),aliyewahi kuwa kiongozi wa Kitongoji cha Kijiji cha Madobore, Kata ya Luponde wilayani Njombe, amedai kucheleweshwa kufa kutokana na kushindwa kutatuliwa kwa mgogoro wa ardhi ya ekari 1,026 uliopo baina ya wakazi wa KIjiji hicho na shirika la watawa la Imiliwaha

Mzee Joseph Gendamwene

Mzee Gendamwene, amesema ana vielelezo vyote vya umiliki wa maeneo yaliyochukuliwa na masista kwa sababu katika kipindi hicho alikuwa kiongozi wa kitongoji ,hivyo anaomba mkuu wa wilaya kufuatilia mgogoro huo kwa kina na haki ipatikane. Eneo hilo lina ukubwa wa ekari 1,026.

Mara baada ya kujipa muda wa kusikiliza upande zinazosigana ,Mkuu wa wilaya ya Njombe Kissa Gwakisa Kasongwa, akaeleza changamoto alizobaini katika umiliki huo na kisha kutoa agizo kwa maafisa ardhi kwenda kufanya tathimini ya eneo lenye mgogoro huku pia akiwataka wananchi na shirika la masista kuwa tayari kwa matokeo.