Mgombea Urais ADC aahidi kufufua vyuo vya ufundi

Ijumaa , 16th Oct , 2020

Mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha ADC, Queen Sendiga amesema kuwa akipatiwa ridhaa ya kuliongoza taifa Oktoba 28, 2020 atahakikisha anavipatia hadhi ya juu vyuo vya ufundi nchini VETA ili kuongeza viwanda.

Mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha ADC, Queen Sendiga.

Bi. Sendiga ametoa kauli hiyo leo wakati akiwahutubia wakazi wa Manzese Jijini Dar es Salaam ambapo amesema kuwa elimu ya ufundi itasaidia kuongeza soko la ajira nchini na kuongeza wabunifu nchini.

Aidha, Sendiga ameongeza kuwa ataondoa vikwazo vilivyopo katika sekta za ajira ambapo wahitimu wengi hukosa ajira kwa kutakiwa kuwa na uzoefu, hivyo katika uongozi wake atalikomesha hilo.

Endapo nikichaguliwa kuwa Rais wa Tanzania, nitaondoa vikwazo vyote katika soko la ajira, masuala ya kuombwa uzoefu wakati umetoka shule hayatakuwepo katika uongozi wangu”, amesema  Sendiga.