Alhamisi , 6th Oct , 2022

Serikali imeziagiza mamlaka za ajira kote nchini kuhakikisha kuwa, zinaendelea kulipa na kutekeleza haki na stahiki zote za watumishi wa umma nchini ikiwa ni pamoja na kutenga bajeti ya kila mwaka ya mafunzo na posho za watumishi kuweza kushiriki michezo kwani ni haki yao kisheria.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora,  Jenista Mhagama,

Maagizo hayo yametolewa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora,  Jenista Mhagama, wakati akifungua rasmi mashindano yanayohusisha Watumishi wa Umma  kutoka wizara, Idara na Taasisi zote za serikali Tanzania (SHIMIWI) yanayofanyika Kitaifa mkoani Tanga. 

Wakizungumza Katibu Mkuu wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali na Afya Tanzania (TUGHE) na Katibu Mkuu wa Shirikisho la Wafanyakazi  (TUCTA), Henry Mkunda, wamesema kuwa vyama hivyo vinaendelea kuwajengea uwezo watumishi kote nchini mara baada ya kustaafu waweze kuendesha maisha yao bila kikwazo chochote. 

Kwa upande wake Afisa Masoko kutoka kampuni ya Agri Com Afrika, inayojihusisha na usambazaji na uuzaji wa zana za kilimo Tanzania Baraka Konkara, amesema wameamua kudhamini mashindano hayo ili kuweza kuboresha afya za wafanyakazi hususani wawapo makazini pamoja na kuwahamasisha wafanyakazi hao kushiriki katika kilimo ili kuweza kujikwamua kimaisha.