Alhamisi , 11th Sep , 2025

Mtuhumiwa alitenda kosa hilo mnamo tarehe 1 Septemba 2025 katika eneo la Funguni Street, Pangani.

Mahakama ya Wilaya ya Pangani, mkoani Tanga imemhukumu kifungo cha miaka 30 jela mtuhumiwa Grayson Muze Msemo (miaka 55), Mkristo, Muinjilisti na mkazi wa Raskazoni Tanga, baada ya kupatikana na hatia ya kosa la kubaka mtoto mwenye umri wa mwaka 1 na miezi 4.

Akisoma hukumu hiyo jana tarehe 10 Septemba 2025 majira ya saa 13:00, Mheshimiwa Husna Mwiula, Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Pangani, alisema kuwa mahakama imeridhika na ushahidi uliowasilishwa na kumhukumu mtuhumiwa kifungo cha miaka 30 jela ili iwe fundisho kwa jamii na kuhakikisha haki inatendeka.              

Awali, imeelezwa mahakamani kuwa mtuhumiwa alitenda kosa hilo mnamo tarehe 1 Septemba 2025 katika eneo la Funguni Street, Pangani.