
Hii inakuja baada ya ugunduzi wa makaburi yanayohusishwa na kanisa la ‘Kufunga hadi Kufa’ huko Shakahola linalotuhumiwa kusababisha vifo vya watu zaidi ya 400 mnamo 2023.
Taarifa zinaeleza kuwa makaburi 21 yanatarajiwa kufukuliwa hii leo katika eneo hilo
Hayo yanajitokeza baada ya hofu kwamba ‘Kanisa la Kufunga hadi Kufa’ huenda bado linaendeleza shughuli zake licha ya Mchungaji wake Paul Mackenzie kuwa kuzuizini.
Mwezi uliopita, mahakama ya Kenya ilikuwa imeamuru kufukuliwa kwa miili inayoshukiwa kuwa ni ya watu ambao walikufa kwa njaa na kukosa hewa kaunti hiyo hiyo ambapo mamia ya washiriki wa kanisa la Mackenzie walipatikana miaka miwili iliyopita.