
Watu hao 13 ambao ni wafanyabiashara wamefariki baada ya kupata ajali ya gari aina ya Fuso ambalo lilipinduka na kudumbukia mtoni katika daraja la mto Njoka lililopo kata ya Namatuhi mkoani Ruvuma
Lori hilo lilikuwa limebeba wafanyabiashara ambao walikuwa wanatokea mnadani kijiji cha Ndongosi na walikuwa wanaelekea kijiji cha Namatuhi.
Kamanda wa polisi mkoa wa Ruvuma ACP Marco Chilya amesema ajali hiyo ilitokea katika daraja la mto Njoka kata ya Namatuhi halmashauri ya wilaya ya Songea mkoani Ruvuma na ilitokea tarehee 9/4/2023 majira ya saa tatu usiku na chanzo cha ajari hiyo ni ubovu wa miundombinu ya barabara ambayo ilisababisha gari hilo aina ya Fuso kupinduka na kuangukia mtoni na kusababisha vifo hivyo vya watu 13 ambao ni wafanyabiashara.
Akiongea na wananchi ambao walifika katika hospitali ya Rufaa ya mkoa Songea kutambua miili ya ndugu zao ambao wamepata ajali mkuu wa mkoa wa Ruvuma kanali Laban Thomas amesema serikali ilipiga marufuku kwa wafanyabiashara kutumia magari ya kubeba mizigo kuwa usafiri wa kuwasafirisha wao hivyo amesema kama wasingetumia usafiri huo vifo vya watu 13 visingeweza kutokea.