Nyufa katika hospitali ya wilaya ya Nsimbo
Mrindoko amefikia hatua hiyo baada ya kukagua mradi huo na kubaini ubadhirifu huo huku ikimlazimu kuamuru wasimamishwe kazi Mhandisi wa wilaya, Afisa Mipango na Mkuu wa Idara ya Afya pamoja na Mkaguzi wa ndani ili kupisha uchunguzi.
Naye Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Mohamed Ramadhani na watumishi wake wa idara wameonesha kutokuwa na uelewa sawa juu ya fedha hizo ,wengine wakidai hawana taarifa na fedha hizo na wengine wakidai ilipelekwa kutekeleza mradi mwingine.
Mhe. Mrindoko ametoa siku saba kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za ndani mkoa wa Katavi kufuatilia taarifa za fedha hizo na ndani ya mwezi apate ripoti ikiwa ni pamoja na TAKUKURU kuchunguza mradi huo.