Ijumaa , 11th Apr , 2014

Rais  mstaafu  wa  awamu ya tatu  Benjamini  Mkapa  amewataka  wananchi  wa  nchi  za  Jumuiya ya Afrika  Mashariki  kutokubali  kuruhusu  chokochoko  za  kikabila, kisiasa  na  kidini  zinazoweza  kuleta  machafuko  na kupelekea  mauaji  ya kimbari.

Rais Mstaafu wa Tanzania Benjamini Mkapa

Rais  mstaafu  wa  awamu ya tatu  Benjamini  Mkapa  amewataka  wananchi  wa  nchi  za  Jumuiya ya Afrika  Mashariki  kutokubali  kuruhusu  chokochoko  za  kikabila, kisiasa  na  kidini  zinazoweza  kuleta  machafuko  na kupelekea  mauaji  ya kimbari  kwani   ni  jambo linalowezekana.

Akizungumza  na  vijana  kutoka  nchi  mbali  mbali  za  jumuiya  ya  Afrika  Mashariki  katika  maadhimisho  ya  kumbukumbu  ya  mauaji  ya  kimbari  yaliyofanyika  Arusha.  Rais mstaafu Benjamini mkapa  amesema  wananchi   hasa  vijana  wanaweza   kuziba mianya  yote  ya  machafuko, lakini  pia  wanaweza  kuwa  chanzo  cha  machafuko  kama  tahadhari  hazitachukuliwa.

Katika  hatua  nyingine  Rais  mtaafu  Benjamini Mkapa  ameishauri  Jumuiya  ya Afrika  Mashariki  kuijengea uwezo  mahakama  ya  Afrika  kwani  ina  nafasi kubwa ya kusaidia kudumisha amani  katika  ukanda  wa  nchi  hizo.

Awali  katibu  mkuu  wa  Jumuiya  ya Afrika  Mshariki  Dkt. Richard  Sazbera  amewataka  viongozi  na  wananchi   wa  jumuiya  ya   Afrika  Mashariki  kuyachukulia  mauaji ya kimbari  ya Rwanda  kama  chanzo  cha  kuepuka  machafuko    na  kudumisha  amani

Maadhimisho  hayo  yaliyohudhuriwa  na  viongozi  na watendaji  mbalimbali  wakiwemo  mabalozi, na  wabunge  wa   Jumuiya  hiyo  yalianza  kwa  maandamano  yaliyopita katika  maeneo mbalimbali  ya jiji  la  Arusha