Jumamosi , 30th Dec , 2017

Mke wa Mwanasiasa maarufu nchi na Mbunge wa Singida Viti Maalum (CHADEMA), Jesca Kishoa leo amtembelea Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu na kusema kwamba wasiojulikana wamemfanya kiongozi huyo kuwa jasiri zaidi.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Mbunge huyo amethibitisha kufika Hospitalini alikolazwa Mbunge Lissu kwa takribani miezi mitatu baada ya kupigwa risasi na watu wasiojulikana Septemba 7 mwaka huu huko mkoani Dodoma.

Mh. Kishoa ameandika " My Brother is fine and Strong..! Shauku yake ya kulitetea taifa hili imeongezeka mara 100000000000..... Aisee ni kama kuzima moto kwa petrol...Wasiojulikana wamemfanya awe jasiri zaidi. Glory to the Almighty God. Aluta Continua"