
Mkurugenzi Mkuu ZAECA, ACP Ahmed Khamis Makarani
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Ijumaa Septemba 2, 2022 na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu-Zanzibar, Charles Hilary, Rais Mwinyi amekubali barua ya kujiuzulu ya Makarani.
Taarifa hiyo imesema hatua hiyo inafuata maelekezo ya Rais Mwinyi kuitaka Zaeca kujitathmini, baada ya hivi karibuni kupokea ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).
Jumamosi ya Agosti 27, 2022, Rais Mwinyi alikabidhiwa ripoti na CAG, Dk Othman Abbas Ali Ikulu Mjini Zanzibar ikianika madudu na ubadhirifu wa fedha za umma.
Akizungumza baada ya kukabidhiwa ripoti hiyo, Rais Mwinyi aliinyooshea kidole Mamlaka ya Kuzuia Rushwa na Uhujumu Uchumi (Zaeca), kuwa haina msaada kwa Serikali.