
Waziri wa Nishati January Makamba kulia na kushoto ni Mkurugenzi wa TPDC Dkt.James Mataragio
Waziri Makamba ameyaeleza hayo, kupitia ukurasa wake wa Twitter ambapo amesema kwamba hakuna uhaba wa mafuta nchini na wala hakuna haja ya kuzua taharuki kuhusu upatikanaji wa nishati hiyo na kwamba serikali inaendelea kuchukua hatua ili kuongeza uhakika wa upatikanaji wake na unafuu wa bei.
"Kauli ya uhakika ni ya serikali, Mkurugenzi wa TPDC atatoa taarifa kuhusu taarifa yake hii manake aliitoa kwenye semina ya wanahabari lakini ni gazeti moja tu ndio limeandika, pia atakuja ofisini kutoa maelezo kabla hatujachukua hatua za ziada," ameandika Waziri Makamba wakati akijibu swali la mwanachi aliyehoji kuhusu mkanganyiko wa taarifa hizo.