Jumapili , 15th Nov , 2020

Mkuu wa Wilaya ya Geita Fadhili Juma, amewataka watendaji wa kata na vijiji kusimamia miradi iliyopo katika maeneo yao kikamilifu.Mkuu wa Wilaya ya Geita Fadhili Juma, amewataka watendaji wa kata na vijiji kusimamia miradi iliyopo katika maeneo yao kikamilifu.

Mkuu wa Wilaya ya Geita Fadhili Juma

Amesema hayo leo akiwa anazungumza na watumishi wa serikali kutoka sekta tofauti kwa lengo la kuwakumbusha kutekeleza majukumu yao kwa manufaa ya wanachi.

                                      Pichani baadhi ya watendaji kutoka maeneo tofauti Wilayani Geita

"Inasikitisha sana unakwenda kwenye kata unamuuliza mtendaji wa kata juu ya miradi na hajui mradi unakwendaje, kama mtendaji wa kata au kijiji unatakiwa ujue kinachoendelea kwenye mradi ulioko katika eneo lako,kama ni fedha au vitendea kazi vinavyohitajika" amesema Fadhil Juma 

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri wa Mji Geita, Mhandisi Modest, Apolinary anasema kupitia ongezeko la madini hayo kumepelekea kuendeshwa miradi  mbalimbali ya maendeleo ikiwemo elimu na afya.

Baadhi ya watendaji wa serikali waliohudhuria kikao hiko wameahidi kwenda kushirikiana na wadau sambamba na wananchi ilikuhakikisha wanatatu matatizo yaliyopo kwenye maeneo yao.