Jumatano , 20th Apr , 2016

Wananchi wa vijiji mbalimbali halmashauri ya wilaya ya Mtwara wamehamasika na kuunga mkono jitihada zinazofanywa na Mkuu wa wilaya ya Mtwara Fatma Ally, za kutatua changamoto ya ukosefu wa madawati katika shule za msingi na sekondari.

Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Fatma Ally, akizungumza na Wanafunzi

Wakizungumza kwa nyakati tofauti katika ziara iliyofanywa na mkuu wa wilaya huyo kwa ajili ya kuhamasisha wananchi kushiriki kikamilifu katika shughuli na mipango mbalimbali ya kimaendeleo, wamesema awali suala hilo lilipokelewa tofauti kwa kujua ni jukumu la viongozi wa ngazi za juu pekee.

Aidha, mkuu wa wilaya ambaye kupitia mfuko wake wa kuhamasisha wananchi kuchangia madawati kwa hiyari aliyouita ‘Haba na haba hujaza kibaba’ ambao mpaka sasa amekusanya sh. Milioni 14, ameagiza ziundwe kamati za watu 10 katika kata Tatu ambazo alizitembelea jana na kuzipa jukumu la uhamasishaji wa suala hilo.

Amesema, kamati hizo zitakuwa na wajumbe watakaowakilisha makundi mbalimbali ikiwa ni pamoja na wazee maarufu wa kijiji, vijana maarufu pamoja na viongozi wao wa vijiji ambapo ameahidi kurudi tena baada ya siku 10 kwa ajili ya kupata mrejesho wa utekelezaji wa maagizo yake.

Sauti ya Mkuu wa wilaya ya Mtwara Fatma Ally,