Alhamisi , 14th Mar , 2024

 Aliyekuwa mmiliki wa Jason's Production, ambao ni waandaji wa Tamthilia maarufu ya (SIRI ZA FAMILIA) iliyokuwa inaoneshwa East Africa TV na 'Country Manager ' wa Wananchi Group , Sanctus Mtsimbe amefariki dunia jana Machi 13, 2024 katika hospitali ya Aga khan alipokuwa akipata matibabu. 

Sanctus Mtsimbe

Taratibu za mazishi zinafanyika nyumbani kwa marehemu Tabata Segerea, Dar es Salaam.

Ndugu Mtsimbe anatarajia kuzikwa  Jumapili hii makaburi ya Mashujaa Kinondoni.

Sanctus ni Mwanzilishi wa group la Consultants, pia alikuwa ndio Rais wa kwanza wa Mtandao wa Wanataaluma Tanzania (TPN), hadi anafariki alikuwa ni Country Manager wa Wananchi Group ambao ndio wamiliki wa Zuku, Simba Net na makampuni mengine.

Ndugu Sanctus pia  alikuwa mjasiriamali na mmiliki wa makampuni kadhaa binafsi , pia mjumbe wa bodi kwa taasisi kadhaa za umma na binafsi.

Kifo chake kimetokea ikiwa ni  mwaka mmoja na miezi kadhaa iliyopita tangu Bwana Mtsimbe alipoondokewa na kijana wake Jason Mtsimbe na yeye jana amefariki dunia