
Bi Truss alijiuzulu siku ya jana ikiwa ni wiki sita tu katika toka aanze kazi hiyo, na kufanya uwaziri wake wenye misukosuko kuwa mfupi zaidi katika historia ya Uingereza.
Wagombea wanaotaka kuchukua nafasi yake wanahitaji uungwaji mkono kutoka kwa wafuasi wa Liz wasiopungua 100, na kupunguza ushindani hadi watatu.
Waziri Mkuu wa zamani Boris Johnson hajaondoa uwezekano wa kugombea tena ikiwa ni miezi kadhaa baada ya kulazimishwa kuondoka baada ya uasi wa Tory.
Wengineo Rishi Sunak na Penny Mordaunt, ambao walisimama bila mafanikio katika kinyang'anyiro cha kuchukua nafasi yake, pia wanaonekana kuwa washindani wa kugombea tena