Jumanne , 2nd Aug , 2016

Mradi wa maji unaohudumia vijiji 50 katika halmashauri ya wilaya ya Wanging’ombe uliojengwa miaka zaidi ya 45 iliyopita umetafutiwa ufadhili kwa ajili ya kukarabati miundombinu yake kwa ufadhili wa dola za kimarekani milioni 87 kutoka nchini India.

Naibu Waziri Wizara ya Maji Mhandisi Gerson Lwenge

Mradi huo unadaiwa kuwa na maji mengi lakini hautosherezi kwa wakazi wake kutokana na miundombinu hiyo kuwa ni ya muda mrefu na kutiririsha maji mengi njiani kabla ya kuwafikia walengwa.

Hayo yamebainishwa na Naibu Waziri Wizara ya Maji, Mhandisi Gerson Lwenge, baada ya madiwani wa halmashauri ya Wanging’ombe kulalamikia kutofikiwa maji kwa wananchi wao ambapo Naibu Waziri huyo halmashauri hiyo ni jimbo lake.

Mhandisi Lwenge anasema kuwa kutokana na mradi huo kuwa ni wa muda mrefu ukarabati unahitajika ili kufkisha huduma hiyo ya maji kwa walengwa na kutoa suluhu ya kudumu ya tatizo hilo katika vijijini hivyo

Kabla ya Naibu waziri kusema hayo madiwani wakahoji upatikanaji wa maji licha ya kuwapo mradi mkubwa Mbukwa ambao maji yake yangetosha kwa vijiji zaidi ya 50.

Sauti ya Naibu Waziri Wizara ya Maji, Mhandisi Gerson Lwenge,