Msanii atembea kwa miguu kutoka mkoani

Ijumaa , 23rd Aug , 2019

Rapa wa nchini Kenya King Kaka, ametembea kwa miguu kutoka mji mkuu wa nchi hiyo Nairobi hadi mjini Nakuru akihamasisha kampeni ya kuchangia taulo za kike.

Rapa wa nchini Kenya King Kaka

Kampeni hiyo itasaidia kuwanunulia wanafunzi wa kike taulo za kike ili kuendelea kubakia shuleni, kama ambavyo East Africa Television na East Africa Radio imekuwa ikifanya kwa mwaka wa tatu sasa.

Safari hiyo ya kutembea kwa miguu ametumia kilomita 154 na siku 6 hadi kufika mjini Nakuru.  

King Kaka amesema anashirikiana na Benki ya "On Me" ili kukamilisha zoezi hilo ambalo lengo lao wanahitaji kuwasaidia wanafunzi Laki moja kubaki shule, na ukichangia shilingi 13,389 utakuwa umesaidia mwanafunzi mmoja kubaki shule kwa mwaka mzima.

Zoezi hilo itaambatana na burudani ya muziki kutoka kwa staa huyo siku ya kesho tarehe 24 ya mwezi wa nane.

King Kaka anafuata nyayo za East Africa Television na East Africa Radio, ambao wameshaanza kampeni hiyo ya kuchangia taulo za kike na tayari wameshafanikisha kutoa taulo hizo za kike katika mikoa mbalimbali na kuwafikia wasichana zaidi ya 5000.