Jumanne , 14th Mar , 2023

Mtoto wa kiume mwenye umri wa miaka tisa mkazi wa Magomeni mtaa wa Mpakani kata ya Ndugumbi anadaiwa kulawitiwa  mara sita huku ikielezwa kuwa mtuhumiwa anayedaiwa kufanya kitendo hicho anaonekana mtaani bila kuchukuliwa hatua za kisheria 

Akizungumza na #EATV mama mzazi wa mtoto huyo jina linahifadhiwa  amethibitisha  kulawitiwa kwa mtoto wake mara baada ya kupeleka hospitali ya rufaa ya mkoa wa Mwananyamala na kufanyiwa vipimo 

Mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Mpakani kata ya Ndugumbi Musa Mwingwa amesema kwamba mtuhumiwa amekuwa akifanya matukio hayo mara kwa mara na kutoweka