Mtoto aelezea kifo cha Dkt Omari Nundu

Jumatano , 11th Sep , 2019

Aliyekuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Simu za Mkononi ya Airtel Tanzania Dkt Omari Rashid Nundu amefariki dunia leo Septemba 11 wakati akipatiwa matibabu ya tezi dume.

Hayati, Dkt. Omari Nundu

Akizungumza na EATV & EA Radio Digital, mtoto wa marehemu anayejulikana kwa jina la Danga Nundu amesema kuwa baba yake amefariki wakati madaktari wakijiaandaa kumfanyia upasuaji kutokana na maradhi yaliyokuwa yanamsumbua.

''Kifo kimetokea leo, alikuwa anafanyiwa upasuaji wa tezi dume ndio presha ikashuka sana na kupelekea mauti yake na alikuwa amelazwa Hospitali iliyoko huku maeneo ya Mbezi Beach'', amesema Danga.

Juni 12, 2019, Dkt Omari Nundu aliteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya kampuni ya mawasiliano ya Airtel.