Kushoto ni Mama mzazi wa marehemu Ibrahim
Kamanda wa Polisi mkoa wa Mbeya, Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP, Benjamin Kuzaga amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kutolea ufafanuzi.
Mama wa marehemu Ibrahim Edson ambaye ni Dafroza Edson ameelezea mazingira ya kifo cha mtoto wake, kwamba alimuaga anaenda kulala chumbani kwake, lakini baadaye dada yake alivyoingia chumbani alimkuta tayari kashajitundika kwenye kamba na mauti yamemfika.








