Mkuu wa Kitengo cha afya ya akili na madawa ya kulevya kutoka hospitali ya rufaa ya mkoa wa Temeke Dkt Francis Lukui Benedict
Dkt. Francis ameyasema hayo hii leo Februari 15, 2023, na kuongeza kuwa asilimia 25 ya wagonjwa wote wanaofikishwa kituo cha kuhudumia watu wenye tatizo la afya ya akili katika hospitali hiyo wametokana na matumizi ya dawa za kulevya zilizosababisha kuharibu mfumo mzima wa ubongo na mwili.
Amesema tatizo ni kubwa tofauti na jamii inavyolichukulia kwani wastani wa wagonjwa 50 mpaka 60 wanaandikishwa kila mwezi kwenye kliniki ya methadone iliyopo katika kituo hicho.
Hata hivyo baadhi ya wananchi wa wilaya ya Temeke wameshauri elimu ya athari za matumizi ya dawa za kulevya ielekezwe zaidi kwenye shule za msingi, sekondari mpaka vyuo Kwa kuwa watumiaji wengi wamebainika kuwa ni vijana


