
Robert Mugabe Jr, mtoto wa aliyekuwa rais wa Zimbabwe marehemu Robert Mugabe, amekamatwa na kufunguliwa mashtaka ya kupatikana na dawa za kulevya baada ya polisi kudaiwa kupata bangi kwenye begi lake wakati akikaguliwa na trafiki mjini Harare.
Mamlaka imesema kijana huyo mwenye umri wa miaka 33 alisimamishwa siku ya Jumatano Oktoba Mosi kwa kuendesha gari kwa njia isiyo sahihi katika barabara ya njia moja. Polisi wanadai waligundua mifuko miwili ya bangi akiwa nayo, huku wanaodaiwa kuwa wanachama watano wanaohusishwa naye pia wakikamatwa wakiwa na bangi pia.
Wakili wa Mugabe amepinga mashtaka hayo, akisisitiza kuwa dawa hizo zilikuwa za abiria wengine waliokuwa kwenye gari tofauti na kuwashutumu polisi kwa kuongeza kiasi cha pesa kilichokamatwa.
Kesi hiyo imevuta hisia kwa sababu ya Mugabe Jr aliepuuza sheria hapo awali. Mnamo 2023, alikamatwa kwa madai ya kuharibu mali na kumtemea mate afisa wa polisi, lakini baadaye akapata suluhu nje ya mahakama. Alirejeshwa rumande siku ya jana Alhamisi huku mahakama ikizingatia ombi lake la kuachiliwa kwa dhamana.
Babake marehemu alitawala Zimbabwe kwa takriban miongo minne kabla ya kulazimishwa kuondoka madarakani mwaka wa 2017. Ingawa uhusiano kati ya familia ya Mugabe na Rais Emmerson Mnangagwa ulidorora baada ya kuondolewa madarakani, Mugabe Mdogo alirudi katika chama tawala nchini humo cha Zanu-PF mwaka 2022 baada ya kuhudhuria mkutano wa chama. #EastAfricaRadio