Alhamisi , 12th Mei , 2016

Halmashauri ya Manispaa ya Musoma na Halmashauri ya jiji la Xiangtang, la nchini China zimesaini mkataba wa mahusiano mema ikiwa ni pamoja na kusaidia katika sekta za elimu, afya, biashara, utalii na uchumi kwa lengo la kudumisha ushirikiano.

Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Manispaa ya Musoma

Hatua hiyo inalenga mahusiano yaliyoanzishwa na waasisi wa mataifa hayo mawili Mwalimu Julius Nyerere na Mao Seitung, katika miongo kadhaa iliyopita.

Zoezi hilo la utilianaji saini limefanyika katika ukumbi wa mikutano wa Manispaa ya Musoma uliopo Mjini Mkoani Mara na kushuhudiwa na viongozi mbalimbali wa nchi hizo wakiwemo mkuu wa wilaya ya Musoma, madiwani, pamoja na ujumbe wa viongozi mbalimbali kutoka nchini humo.

Akizungumza wakati wa zoezi la utilianaji saini huo Meya wa Manispaa ya Musoma, Bw. Wilium Gumbo, amewahakikishia wageni kuwa Manispaa ya Musoma ipo tayari kuendeleza mahusiano yaliyoanzishwa na waasisi wa mataifa hayo ikiwa ni pamoja na kuwahakikishia wageni hao kuja kuwekez.

Amesema kuwa mji wa Musoma unamazingira yanayowezesha uendeshaji wa shughuli za kibiashara na kiuchumi huku meya wa jiji la XIANGTAN akiahidi kutoa fursa za kiuchumi na kielimu, utalii, pamoja na utamaduni.

Kwa upande wao madiwani wa Manispaa ya Musoma Bw. Ahmad Kitombo na Bi Rebeca Mkama wakaelezea furaha yao huku wakiahidi kudumisha ushirikiano uliopo.