Jumatano , 14th Oct , 2020

Wafanyabiashara zaidi ya 20 katika soko la Veternary wameeleza namna walivyopata hasara baada ya mapaa ya mabanda yao kuezuliwa  na upepo uliotokana na  mvua iliyonyesha hapo jana.

Wafanyabiashara katika Soko la Veternary wakiezeka upya mapaa ya mabanda yao baada yakuezuliwa na upepo.

Wakiongea na Kurasa leo wafanyabiashara hao ambao leo wamekuwa wakiezeka upya mabanda hayo wamesema wamepoteza zaidi ya shilingi milioni moja kwa kila mmoja wao kwa kuwa upepo huo ulioambatana na mvua ulisababisha maji kujaa katika eneo hilo la soko.

"Tatizo hili ni la mda mrefu na viongozi wanalifahamu lakini tunashangaa kwamba hatusaidiwi licha ya viongozi kuliona" amesema Egidius Mfanyabiashara soko la Veternary

Naye katibu wa soko hilo Erasmus  Ngombo, amesema kuna haja sasa kwa serikali hasa manispaa kuwajengea wafanyabiashara hao mabanda ya kudumu ili kuwaepusha na hasara wanazozipata kila mara mvua inaponyesha.