Jumanne , 31st Jan , 2023

Jeshi la DRC limesema kwa sababu za kiusalama limewaamuru kuondoka nchini humo maafisa wa Rwanda waliokuwa wanachama wa Kamandi ya Vikosi vya Kanda ya Jumuiya ya Afrika Mashariki iliyoko Goma, DRC.

Katika taarifa, msemaji wa jeshi Jenerali Maj Sylvain Ekenge amesema maafisa hao tayari wameondoka katika ardhi ya Congo.

Taarifa kutoka kwa msemaji wa jeshi la Rwanda Brig. Jenerali Ronald Rwivanga Rwanda ndiyo iliwaita maafisa hao

kwa upande wa DRC imewakataa wanajeshi wa Rwanda kuwa sehemu ya wanajeshi wa kanda linaloongozwa na Kenya waliotumwa mwaka jana katika jimbo la Kivu Kaskazini nchini DRC.

Mvutano kati ya Kigali na Kinshasa umezidi kuwa mbaya wiki iliyopita wakati jeshi la Rwanda lilipopiga kombora ndege ya kivita ya Congo karibu na uwanja wa ndege wa Goma. Utaratibu wa uthibitishaji wa kikanda umewekwa ili kuchunguza tukio hilo.