Mwenyekiti wa Kijiji cha Old Shinyanga Dotto Bwire amesema alipata taarifa usiku majira ya saa saba na kwenda eneo la tukio ambapo alikuta Jeshi la zimamoto na uokoaji Mkoa wa Shinyanga wakiwa tayari wamefanikiwa kuudhibiti moto huo licha ya kuteketeza vitu vilivyokuwa sebuleni
Inaelezwa kuwa mama mzazi wa marehemu wakati tukio linatokea alikuwa hospitali kuuguza mgonjwa
Kwa upande wake Mkuu wa Jeshi la zimamoto na uokoaji Wilaya ya Shinyanga Inspekta Stanley Luhwago amesema walipata taarifa usiku huo na kuwahi eneo la tukio ambapo walifanikiwa kuzima moto huo kabla ya kuendelea kusambaa kwenye nyumba nzima na vyumba vya wapangaji








