
William Malecela maarufu kama Lemutuz enzi za uhai wake
Taarifa za kifo cha mtoto huyo wa Waziri Mkuu wa zamani wa Tanzania John Malecela zimethibitishwa na Ofisi yake ya Lemutuz Online TV na baadhi ya watu wake wa karibu.
#TANZIA Mfanyabiashara wa maudhui ya mtandaoni William Malecela maarufu kama Lemutuz ambaye ni Mkurugenzi wa Lemutuz Online TV, amefariki dunia leo Mei 14, 2023.
Wasanii na watu maarufu mbalimbali wamepost taarifa za kifo hicho huku wakieleza mshtuko na masikitiko yao. pic.twitter.com/06ykLdsrbR
— EastAfricaTV (@eastafricatv) May 14, 2023
Meneja wa Lemutuz Online TV, Deusdedith Innocent amesema kifo hicho kimetokea jijini Dar es Salaam huku akibainisha kuwa wanasubiri taarifa rasmi ya familia itakayoeleza zaidi kuhusu msiba huo.
Wasanii na watu maarufu mbalimbali nchini wamepost taarifa za kifo hicho huku wakieleza mshtuko na masikitiko yao.
Taarifa zaidi tutaendelea kukuletea endelea kufuatilia.