Jumanne , 30th Mei , 2017

Mwanamke mmoja aliyefahamika kwa jina la Siyajui Almasi mkazi wa kijiji cha Mahembe, Wilayani Kigoma amenusurika kufa baada ya mume wake aliyetambulika kwa jina la Maguru Shabani kumchoma kisu shingoni.

Kwa mujibu wa taarifa zilizopo zinasema kuwa mume wa Siyajui alimchoma mke wake kisu shingoni akiwa na lengo la kutaka kumuua kutokana na wivu wa mapenzi lakini lengo lake hilo halikutimia baada ya mwanamke huyo kupata msaada.