
Akizungumza na vyombo vya habari Kamanda wa polisi Mkoa wa Njombe Hamis Issa anasema hadi sasa mwili wa mwananke huyo umehifadhiwa katika hospitali ya mji Njombe Kibena na kisha kutoa rai kwa wananchi Kwenda kuangalia mwili huo ili uchukuliwe na ndugu.
Katika hatua nyingine Kamanda Issa amewataka wamiliki wa shule binafsi kupeleka mara moja mabasi yanayobeba Watoto kukaguliwa ili kulinda usalama wao wa watoto.