
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mh. Aggrey Mwanri, akitoa somo la fursa kwa baadhi ya wananchi wake
Akizungumza katika mafunzo maalum ya waratibu elimu kata wa mkoa huo wilayani Urambo Mwanri amesema tangu mpango huo ulipoanza utekelezaji wake mwaka 2015 umeanza kusaidia mkoa hadi kushika nafasi ya 10 kitaifa mwaka huu kutoka nafasi ya mwisho kwa miaka minne mfululizo.
Mkuu huyo wa Mkoa amesema usimamizi mbovu wa watoto hapo awali ulikua unawafanya watoto wengi kutumikishwa katika kazi mbalimbali mkoani humo hali iliyokuwa inafanya washindwe kuzingatia masomo na wengine kuacha kabisa shule.
Mwanri amesema kuwa mkoa wa Tabora watoto wengi wanatumikishwa kwenye mshamba ya tumbaku,mashamba ya mpunga pamoja na migodi hivyo amewataka wazazi wawe na mahusiano mazuri na walimu ili kuboresha sekta ya elimu katika mkoa huo.