Jumatano , 1st Sep , 2021

Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe na wenzake watatu wamefikishwa katika Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi, kwa ajili ya kusikiliza uamuzi dhidi ya pingamizi walilowasilisha mahakamani hapo la kupinga kesi yao kusikilizwa na mahakama hiyo.

Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe Mahakamani

Washtakiwa hao wamefikishwa mahakamani hapo, leo Septemba Mosi, 2021 majira ya saa mbili asubuhi na kupelekwa mahabusu iliyopo mahakamani hapo na baadae kupelekwa ndani ya ukumbi wa mahakama, kwa ajili ya kusikiliza uamuzi wa Jaji  Luvanda.

Jana Agosti 31, 2021 Mbowe na wenzake waliwasilisha pingamizi mahakamani hapo wakipinga mahakama hiyo kusikiliza kesi yao kwa mashtaka ya ugaidi na kwamba kwa mujibu wa Sheria ya Kuzuia Ugaidi kesi yao inapaswa kusikilizwa na Mahakama Kuu ya kawaida na si hiyo ambayo ni divisheni maalumu.

Tazama Video hapo chini