
Sehemu ambayo mwili wa kichanga umeonekana
Kulingana na wakazi hao, mwili huo ulikuwa bado mbichi, ishara kwamba ulikuwa umezaliwa saa chache mapema, pengine Jumamosi usiku.
Kufuatia tukio hilo , Mwenyekiti wa eneo la Nyumba Kumi Joel Githinji, amepinga kitendo hicho kwa kukitaja kuwa cha kikatili na amewataka wanawake kukubali majukumu ya uzazi pindi wanapobaini ni wajawazito badala ya kutoa mimba zisizotarajiwa kwani zinaweza kuhatarisha maisha yao.
Pia amewashauri waepuke uhusiano na wanaume wasiowajibika na wapenda starehe za mwili tu kwani hawawezi kubeba majukumu ya wazazi.