Jumapili , 26th Jun , 2022

Waziri wa TAMISEMI Innocent Bashungwa, amesema jumla ya nafasi 736 kada za afya zimekosa waombaji wenye sifa, kada hizo ni Daktari wa Meno 50, Tabibu Meno 43, Tabibu Msaidizi 244, Mteknolojia Mionzi 86 na Muuguzi- ngazi ya cheti 313.

Waziri wa TAMISEMI Innocent Bashungwa

Taarifa hiyo imetolewa leo Juni 26, 2022, jijini Dodoma na Waziri Bashungwa, wakati akaitangaza matokeo ya ajira 9,800 za walimu wa shule za msingi na sekondari pamoja na na nafasi 7,612 za wataalam wa afya.

"Kada hizi zitarudiwa kutangazwa ili kupata waombaji wenye sifa watakaojaza nafasi hizi," imeeleza taarifa ya Waziri Bashungwa