Jumanne , 13th Feb , 2018

Naibu waziri wa maji Mhe Jumaa Aweso ameagiza mhandisi wa manispaa ya Temeke Damas Shirima kukamatwa na kuhojiwa na polisi kwa kosa la kutoa maelezo yasiyo ridhisha juu ya utekelezaji wa mradi wa maji wa mwasongo uliopo Kigamboni Dar es salaam.

Akizungumza katika majumuisho ya siku yake ya pili ya ziara yake jijini Dar es salaam Mhe Aweso amesema kuwa serikali haiwezi kunyamaza kimya pale inapooneka miradi ya maji inahujumiwa waziwazi na kwamba watahakikisha wale wote ambao wanagundulika kuhujumu miradi ya maji hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.

Awali mbunge wa jimbo la Kigamboni ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya Dkt. Faustine Ndugulile amesema kuwa jimbo lake bado linachangamoto ya upatikanaji wa maji kwa baadhi ya maeneo ambapo amehaidi kulisimamia suala hilo ili wananchi waondokane na kero hiyo.