
Kamishna wa TRA aliyesimama.
Kamishna Kichere amebainisha hayo leo Mei, 17, 2019 kwenye kikao cha pamoja na mameneja wa TRA mbalimbali ambapo amewataka kutoa huduma ipasavyo kwa walipakodi.
Kichere ameeleza kuwa wafanyakazi wanaofanya kazi kwa mazoea ni wale wanaokwepa kusikiliza kero za walipakodi kwa wakati, hivyo kusababisha usumbufu.
''Ufanyaji kazi kwa mazoezi haufai kwenye mamlaka yetu, naagiza kila meneja kuweka namba za simu nje ya ofisi yake ili walipakodi waweze kuwasiliana nao wanapokuwa na jambo linalowakwaza'', - amesema.