Alhamisi , 17th Jan , 2019

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai ameeleza kwamba ni lazima Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Serikali, Prof. Mussa Assad  aweze kwenda kuhojiwa kwenye Kamati ya Maadili  na asipokwenda atamuonyesha yupi ni bosi wake.

Kushoto ni Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Serikali, Prof. Mussa Assad, Spika Job Ndugai kulia.

Akizungumza na vyombo vya habari leo, Spika Ndugai amesema kwamba CAG siyo muhimili kama jinsi ambavyo anakuzwa na baadhi ya watu na badala wake yeye ni Ofisa anayefanya  kazi za kuchunguza kazi ambazo zilitakiwa zifanywe na wabunge.

Akizungumzia kuhusu kinga ya Ndugai amesema suala la maadili haliangalii kuhusu cheo hata akiwa yeye mwenyewe haruhusiwi kuizungumza vibaya nchi yake akiwa nchi nyingine kwani maadili hayaruhusu.

"Hata awe nani? msichanganye vitu, hii haina exception, ndiyo maana wanaoapishwa na Rais lazima wasome kiapo cha maadili.  Ni maadili unatoka nje ya nyumba alafu unaanza kwamba ooh mke wangu mimi.....kuna madili hapo?. Ni maadili atakuja tu na litaisha" Ndugai.

Ameongeza kwamba wale wanaotoa mifano kuhusu CAG wa Uganda bi waongo kwa kuwa alishawasiliana na mamlaka za huko.

"Waganda wameniambia 'that is a big fact Lie'. Kule Uganda System yake ni ile ya 'Common Wealth CAG' ni ofisa wa bunge . Hata Kenya unadhani Ofisa wa bunge anaweza kumgomea Spika? hii mifano anaitoa wapi? anawakuzwa sana?. Mihimili ni mitatu huu wa nne unatoka wapi?" amesema Ndugai.