Jumatano , 31st Mei , 2017

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Job Ndugai amemtumia salamu za rambirambi Mwenyekiti wa CHADEMA, Mh. Freeman Mbowe, kufuatia kifo cha Mzee Ndesamburo kwa kuweka wazi kwamba ni kiongozi ambaye alikua mchapakazi kwa wananchi wake.

Kushoto ni Philemoni Ndesamburo (Marehemu), Kulia ni Spika Job Ndugai

“Nimepokea kwa masikitiko taarifa ya kifo cha Mh. Ndesamburo ambaye pia ni baba wa Mbunge wa Viti Maalumu Lucy Owenya kilichotokea mkoani Kilimanjaro hakika ni pigo kubwa” Alisema

Aidha Mh. Ndugai amesema kuwa marehemu Ndesamburo, aliyewahi kuwa mbunge wa jimbo la Moshi mjini mwaka 2000 - 2015 atakumbukwa kwa uchapakazi wake wakati akiwa mbunge hasa katika kuwaletea wananchi wa jimbo lake maendeleo.

Mhe. Ndesamburo aliyezaliwa 19 Februari 1935, amefariki leo tar 31 Mei 1935 akiwa hospitali ya KCMC mjini Moshi huku taarifa za chanzo cha kifo chake kikiwa bado hakijabainika