Alhamisi , 13th Jun , 2019

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imesema kuwa itaanza uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura kuanzia mwezi Julai kwa njia ya Kielektroniki (BVR) pamoja na kutaka wapigakura waliokwisha jiandikisha kwenda kwa ajili ya kupewa kadi mpya.

Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi, Jaji Semistocles Kaijage

Taarifa hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa tume hiyo, Jaji Semistocles Kaijage leo Jijini Dar es Salaam katika mkutano uliowakutanisha viongozi wa vyama vya siasa wenye lengo la kujadiliana jinsi ya kuboresha daftari la kudumu la wapigakura watakaoshiriki uchaguzi mwaka 2020.

Jaji Kaijage ameongeza kuwa zoezi la uboreshaji daftari la wapigakura linaambatana na utoaji wa elimu kwa wananchi huku akitoa maelekezo kwa wale ambao wamehama katika maeneo yao ya makazi ya awali walipojiandikisha, kuharibu ama kupoteza kadi zao.