Tamko la mtandao huo watetezi wa haki za binadamu linakuja mara baada notisi liyotolewa na msajili mashirika yasiyo ya kiserikalj Februari 23 mwaka huu iliyoeleza mashirika 2915 kuwa yapo pia hatarini kufutwa kwa kushindwa kuwasilisha taarifa zao kwa zaidi ya miaka miwili pamoja na kushindwa kulipa ada ya mwaka.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Afissa uchechemuzi wa mtandao huo Nuru Maro amesema licha ya changamoto zinazoyakumba mashirika hayo hivyo yana wajibu kufuata kanuni.
Akieleza changamoto zinazokumba mashirika hayo wakili wa mtandao Paul Kisabo amesema mashirika mengi yamekuwa yakishindwa kutoa taarifa ya mwaka pamoja na kulipia ada ya mwaka huku yakiwa yanakabiliwa na ukosefu wa fedha na kudhaniwa yanakiuka sheria.
Aidha ametoa wito kwa wafadhili kuzingatia uwiano wa rasilimali wanazotoa kwa mashirika yote na kutokuwa na upendeleo kwa baadhi ya mashirika na kuyasihi mashirika hayo kuomba ruzuku kwa makundi ili kuweza kupata ruzuku za kuendesha shughuli zao.
Amesema idadi ya mashirika hayo yaliyo hatarini kufutiwa usajili inaweza fanya jumla ya mashirika yasiyo ya kiserikali yatakuwa yamefutiwa usajili kuwa 7794 ikiwa ni pamoja na yale 4879 yaliyofutiwa usajili Januari 24 mwaka huu.








