Alhamisi , 24th Nov , 2022

Mwenyekiti wa UWT wilaya ya Kigamboni jijini Dar es Salaam, Lilian Wasira, amemuombea radhi kwa Watanzania na kwa Rais Samia Dkt Bashiru Ally, aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa CCM, kufuatia kauli yake aliyoitoa hivi karibuni ya kwamba Rais Samia haupigi mwingi.

Mwenyekiti wa UWT wilaya ya Kigamboni jijini Dar es Salaam, Lilian Wasira

Kauli hiyo ameitoa wakati akizungumza kwenye kipindi cha Mamamia cha East Africa Radio na kuwaomba Watanzania wamsamehe akiamini kwamba Dkt. Bashiru aliteleza.

"Tunasema mkubwa hakosei anateleza tu, Mhe (Dkt. Bashiru) ameteleza namuombea radhi kwa Mama Samia na Watanzania wamsamehe ila waipuuze ile kauli, ila kama ile kauli alimaanisha na anahisi hakuteleza basi sisi kina mama tutam-dissapoint, sisi akina mama hatutakubali," amesema Mwenyekiti huyo